| Cecilia Mfuko - Ikwiriri FDC |
Mkuu wa chuo cha IKWIRIRI FDC mama Cecilia Mfuko amepokea
gari moja kutoka kwa Mbunge wa Rufiji Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa. Gari hilo lilikuwa limeombwa kwa Mbunge huyo
katika siku za nyuma na Mbunge alipokea ombi hilo na akakubali kulifanyia kazi.
Siku ya jana tarehe 24 May 2016 katika sherehe za kupokea mwenge hapa chuoni, katibu wa Mbunge Mheshimiwa
Mohamed Mchengerwa katika hotuba yake alisema kuwa Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ametoa gari moja
kwa ajili ya mafunzo ya udereva katika chuo cha IKWIRIRI FDC.
No comments:
Post a Comment