Chuo cha maendeleo ya wananchi Ikwiriri (IKWIRIRI FDC) sasa kinatoa
mafunzo ya kozi ya computer ya muda mrefu yaani miaka miwili na kwa muda mfupi
yaani miezi mitatu.
Unapomaliza kozi hii unakuwa na
uwezo mkubwa wa kufanya mitihani ya VETA hapahapa chuoni ili kufungua wigo
mkubwa wa kuendelea na masomo na kupata ajira katika taasisi za kiserikali au
zisizo za kiserikali.
Katika kuhakikisha mwanfunzi
anaelewa vizuri, mwanafunzi anapewa komputa ya mazoezi katika chumba cha
komputa cha chuo ambapo atafanya mazoezi ya kutumia komputa muda wote wa
masomo.
Chuo kinatoa wito mkubwa kwa wanajamii
wajitokeze kusoma computa kwa ajili ya masomo ya baadaye na kukabili changamoto
za kila siku.
No comments:
Post a Comment