ADMISSION

TANGAZO LA KUJIUNGA NA MASOMO KATIKA FANI ZA UFUNDI KWA MWAKA WA MASOMO 2018

Chuo cha IFDC kimetoa nafasi za kujiunga na fani mbalimbali mwaka wa masomo 2017. Ili kupata tangazo kamili download hapa chini.

TANGAZO LA MASOMO - IFDC_ICT LEVEL 3 Download Hapa

IFDC_Application _form - (kiswahili)_Download Hapa
IFDC_ICT Application _form (LEVEL 3)_Download Hapa Download hapo juu

NGAZI ZA ELIMU ZITOLEWAZO CHUONI
Chuo cha IKWIRIRI FDC kinatoa elimu katika ngazi za viwango vya elimu ya ufundi hapa nchini Tanzania, yaani “National Technical Awards (NTA)” Viwango hivi vimelenga kupima utumiaji mahili wa ujuzi na maarifa yanayotolewa katika sekta husika. Mfumo wa NTA una levo saba ukiunganisha na levo tatu za mfumo wa VETA unaojulikana kama “National Vocational Awards (NVA)” . Kwa hiyo chuo kinatoa NVA LEVEL 1 kwa mwaka wa kwanza, NVA LEVEL 2 kwa mwaka wa pili na NVA LEVEL 3 kwa mwaka wa tatu kama inavoonesha katika jedwali hapa chini.

Level
Award
NVA    1
Certificate of Competence - Level I
NVA    2
Certificate of Competence - Level II
NVA    3
Certificate of Competence - Level III


Baada ya hapo mwanachuo anaweza kujiajiri ama kuajiriwa ama kuendelea na masomo katika ngazi ya NTA LEVEL 4 na kuendelea katika vyuo vya ufundi kama vile CHUO CHA UFUNDI MBEYA, CHUO CHA UFUNDI DAR ES SALAAM, CHUO CHA MADINI DODOMA na vyuo vingine vya ufundi nchini Tanzania

JINSI YA KUJIUNGA NA CHUO CHA MAENDELEO IKWIRIRI FDC


Taratibu za kujiunga na chuo ni kwamba kwanza yanatolewa matangazo kwa kubandikwa kwenye mbao za matangazo kwenye ofisi mbalimbali, katika wilaya ya Rufiji na pia kwenye makanisa na misikitini. Anayetaka kujiunga huchukua fomu na baadae kufanya usaili.

SIFA ZA UDAHILI
Chuo cha IKWIRIRI FDC kinadahili wanachuo kwa utaratibu ambao unafahamika tayari kwa watanzania wote. Sifa za mwanachuo kudahiliwa chuoni ni kama ifutavyo.
a)     Elimu ya shule ya msingi darasa la saba (kwa baadhi ya kozi)
b)    Elimu ya sekondari ya kidato cha nne (kwa kozi zote)
c)     Mtu aliyekaa kiwandani na kupata uzoefu kwa zaidi ya mwaka mmoja - Apprentices from the industry with field experience for one year (kwa baadhi ya kozi)
MUDA WA UDAHILI
Chuo kinadahili wanachuo wa kozi za muda mrefu mara moja tu kwa mwaka. Zoezi la udahili linaanza mwezi wa kumi wa kila mwaka kwa kutangaza na kutoa fomu za maombi katika sehemu mbalimbali za wilaya na katika mtandao wa chuo. Na mwezi wa kwanza zoezi la udahili linakuwa limeshakamilika na masomo kuanza.
Wanafunzi wa kozi za muda mfupi wanadahiliwa muda wowote pale ambapo hitaji linapokuwa limehitajiwa na jamii inayotuzunguka.
SIFA ZA KUJIUNGA NA CHUO (ENTRY REQUIREMENTS) KWA KOZI ZA MUDA MREFU
KOZI (COURSE PROGRAM)
SIFA (REQUIREMENTS)
1
MOTOR VEHICLE MECHANICS
(UFUNDI MAGARI)
a)   O level secondary education.
2
MASONRY AND BRICKLAYING – CIVIL ENGINEERING
(UJENZI)
a)   Ordinary Secondary School Education
b)   Apprentices from the industry with field experience in Masonry and Bricklaying for one year
3
COMPUTER
(KOMPUTA)
a)   Ordinary Secondary School Education
b)   Apprentices from the industry with field experience in computer for one year
4
COOKERY
(MAPISHI)
a)      Primary school Standard VII certificate
b)      Ordinary Secondary School Education
c)      Apprentices from the industry with field experience in cookery for one year
5
TAILORING
(USHONAJI)
a)      Primary school Standard VII certificate
b)      Ordinary Secondary School Education
c)      Apprentices from the industry with field experience in Tailoring for one year
6
DOMESTIC ELECTRICITY
(UMEME WA MAJUMBANI)
a)        Primary school Standard VII certificate
b)        Ordinary Secondary School Education
c)         Apprentices from the industry with field experience in electricity for one year
7
AGRICULTURE, ANIMAL HUSBANDRY AND POULTRY PRODUCTION
(KILIMO NA MIFUGO)
a)        Primary school Standard VII certificate
b)        Ordinary Secondary School Education
c)         Apprentices from the industry with field experience in agriculture for one year
8
HOTELI
(HOTEL MANAGEMENT)

a)     Ordinary Secondary School Education
b)      Apprentices from the industry with field experience in hotel management for one year

SIFA ZA KUJIUNGA NA CHUO (ENTRY REQUIREMENTS) KWA KOZI ZA MUDA MFUPI

Kwa kozi za muda mfupi mwanachuo anaweza kuwa na sifa yoyote katika sifa tajwa hapo juu na kusoma kozi yoyote katika kozi taja hapo juu. Hii ni kwa sababu kozi ya muda mfupi inakuwa ni mafumzo maalumu katika kozi husika, ambayo yatampa ujuzi mwanachuo ili aweze kufanya kazi fulani katika mazingira yanayomzunguka.

No comments:

Post a Comment