Mkuu wa chuo Mama CECILIA MFUKO alikutana na baraza la chuo kuongea na wanachuo na watumishi wote katika siku ya kufunga muhula wa kwanza wa masomo tarehe 17/6/2016. Mkuu alitoa nasaha nyingi kwa wanachuo ili wawe makini pindi wanapokuwa nyumbani kwa ajili ya mapumziko mafupi. Pia aliwasisitiza wanachuo pindi watakapofungua chuo wanapaswa kuja na mahitaji yote yanayostahiki ikiwa ni pamoja na ada ya chakula.
No comments:
Post a Comment