Chuo cha IKWIRIRI FDC kilianzisha mafunzo kwa wasichana
waliosimamishwa masomo kutokana na kupata ujauzito wakiwa shule (shule ya
msingi na sekondari). Mafunzo hayo ya ufundi mbalimbali yaliitwa “Mama Course”.
Mpango huu wa kuwasaidia wasichana hawa umekuwa ukidhaminiwa na wadau wa elimu;
Karibu Tanzania Association (KTA). Kama chuo tunatoa shukrani za dhati kwa
taasisi hii kwa tutoa msaada huo kwa watoto hawa. Lakini pia tunapenda
kuwaalika wadau wengine kuja na kujitokeza kuwasaidia wasichana hawa kwani wapo
wengi sana katika maeneo yanayozunguka chuo, lakini pia Tanzania nzima kiujula.
Wadau wa elimu na wasio wa elimu wa sekta za serikali na sekta binafsi
wanakaribishwa kutoa michango yao ili kuwasaidia watanzania hawa kukamilisha
ndoto zao za kimasomo na kimaisha.
![]() |
wanafunzi wa Mama Course, walimu na Mkuu wa Chuo (watatu kutoka kulia) |
Asante.
No comments:
Post a Comment