Tuesday, May 31, 2016

UKAUSHAJI WA MBOGA ZA MAJANI NA MATUNDA

IKWIRIRI FDC leo ilikuwa inatoa mafunzo ya ukaushaji wa mboga za majani na matunda (papai) kwa vikukndi vya akina mama. lakini pia walimu waliwafundisha akina mama hao umuhimu wa matunda katika mwili wa binadamu. hasa walikazia katika Vitamin A na Vitamini C. kwani vitamini A huondoa tatizo la macho kutoona vizuri na vitamini C husaidia kuimarisha mifupa na kuimarisha kuta za mishipa ya damu. 
lakini pia walimu waliwafundisha akina mama hao waliokuwa wameambatana na akina dada juu ya madhara yanayosababishwa na ulaji wa chipsi za kukwaangwa uliokithiri. kwani husababisha mwili kutunza mafuta ya ziada yatokanayo na chipsi hizo katika matiti na tumbo la chini (kitambi). hii husababisha mimba changa kuharibika. 
akina mama hao walielewa somo vizuri na wakamshukuru mkuu wa chuo kwa mafunzo hayo.


wakufunzi; Elieth (kushoto) na Dororosa (kulia) wakitoa maelekezo kwa wanajamii ya Ikwiriri.










No comments:

Post a Comment