Tuesday, August 16, 2016

UGENI WA MKUU WA MKOA WA PWANI – IKWIRIRI FDC
Jana mkuu wa chuo (Cecilia R mfuko), alipata ugeni kubwa wa Mh Mkuu wa mkoa na Mh Mkuu wa Wilaya. Mkuu wa mkoa aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zinazokikabili chuo chetu kama ifuatavyo.


1. Changamoto ya mgogogoro wa ardhi, Mh Mkuu wa Mkoa  aliagiza Uongozi wa Wilaya ya Rufiji ukae na uongozi wa kijiji cha Ikwiriri kusini na kushughulikia suala la mgogoro wa ardhi na liishe mapema kwani limekuwa ni la muda mrefu.

2. Changamoto ya Computer na Projector, mh. Mkuu wa Mkoa alisema kwamba ataongea na wawekezaji wa mkoa wa Pwani ili wasaidie kutoa computer na projector hapa chuoni kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.

3.Changamoto ya majengo chakavu, Mh Mkuu wa mkoa alisema kuwa ataongea na Mh. Waziri husika ili kumaliza kabisa changamoto hii.


4.Changamoto ya kozi ya udereva (driving school), Mh Mkuu wa mkoa alifurahi sana kwani katika mkoa wa pwani na hasa wilaya ya Rufiji kumegubikwa na vijana wanaondesha bodaboda na magari bila ya leseni ya udereva. Na hivyo amemuagiza OCD kushirikiana na chuo ili kumaliza kabisa TATIZO HILI, kwani litapunguza ajali na vifo kwa vijana wetu.


No comments:

Post a Comment